Utafiti pia umegundua kwamba,dawa nyingine ambayo hutumika kupunguza madini chuma mwilini iitwayo Deferiprone,nayo pia inaweza kupambana na kutokomeza kabisa virusi vya ukimwi kwenye mchanganyiko maalum wa kimaabara uliokuwa umepandikizwa virusi vya ukimwi.Napo baada ya dawa kusitishwa virusi vya ukimwi havikuweza kurudi tena kwenye mchanganyiko huo.
Kumbuka kuwa dawa za sasa za kurefusha maisha kwa waathirika wa ukimwi hazina uwezo wa kutokomeza kabisa virusi hivyo na mgonjwa anapositisha dozi virusi hivyo huzaliana tena.
Watafiti hao kutoka chuo cha tiba cha New Jersey cha nchini marekani waliandika utafiti wao kwenye jarida la PLOS ONE.
Dawa hizi mbili tayari zinatumika kwa matumizi ya binadamu(japo si kwa kutibu ukimwi),hivyo kuziendeleza mpaka zitibu ukimwi inasemekana kutatumia bajeti ndogo na muda mfupi.
Daferiprone yenyewe kwa kuwa ni ya kunywa,imejithibitisha kuwa ni salama ndani ya mwili wa binadamu hivyo majaribio ya dawa hii katika kutibu ukimwi tayari yameanza moja kwa moja kwa binadanu bila kupitia hatua ya awali ya kujaribu kwa wanyama.Majaribio hayo yanafanyika nchini afrika kusini.
0 comments:
POST A COMMENT