Historia ya kigiriki inatuaminisha kuwa alama ya fimbo na nyoka inawakilisha fimbo ya Asclepius,Asclepius alikuwa ni mungu wa kigiriki wa tiba na uponyaji.Sanamu kadhaa za Asclepius zinamuonesha akiwa amebeba fimbo yake ikiwa imezungukwa na nyoka.
Enzi za kale Wagiriki walikuwa wakiingia kwenye mahekalu ya mungu wao wa tiba na uponyaji,Asclepius kwa ajili ya kupata msaada wa magonjwa yaliyowasumbua.Usiku walilala kwenye hilo hekalu wakiamini kwamba mungu mwenyewe,Asclepius angewashauri nini cha kufanya kurudisha afya zao kupitia ndoto.Nyoka wasio na sumu waliachiliwa watambae kwenye sakafu ambayo wagonjwa na waliojeruhiwa walilalia.Ndoto yeyote itakayootwa siku hiyo innaripotiwa kwa kiongozi wa dini ambaye yeye anaelekeza tiba kulingana na tafsiri ya hiyo ndoto.Nyoka pia walitumika kwenye shughuli nyingine nyingi za kitiba na kiimani zilizomuhusisha Asclepius.Kutokana na imani na matumizi makubwa ya nyoka kwenye tiba na uponyaji,inaonekana wafuasi wa Asclepius,mungu wa tiba waliamua kumuweka nyoka kwenye fimbo ya mungu wao(sanamu).
NADHARIA NYINGINEZO
Kuna aina ya mnyoo unaitwa mnyoo wa guinea"dracunculus medinensis".Mnyoo huo hutokeza kwenye kidonda kinachouma sana.Tiba ya kiasili ya tatizo hili ni kuuvuta mnyoo kutoka kwenye kidonda kwa kuuviringisha kwenye kijiti.Alama ya nyoka na fimbo vimefananishwa na mnyoo wa guinea ulioviringishwa kwenye kijiti
Nadharia nyingine kuhusu alama ya fimbo na nyoka inatoka kwenye Biblia kitabu cha HESABU 21:8-9"Bwana akamwambia Musa,jifanyie nyoka ya shaba,ukaiweke juu ya mti,na itakuwa kila mtu aliyeumwa,aitazamapo,ataishi.Musa akafanya nyoka ya shaba,akaiweka juu ya mti,hata ikiwa nyoka amemwuma mtu,alipoitazama ile nyoka ya shaba,akaishi"
Las Vegas Casino Map & Directions - Mapyro
ReplyDeleteLas 인천광역 출장안마 Vegas Casino 수원 출장샵 Address, 3131 South Las Vegas 경기도 출장샵 Boulevard, Las 대구광역 출장샵 Vegas, NV 89109. 포커 족보 Phone Number, 1-702-8900, Toll Free 800-852-7000,