MATUMIZI YA EARPHONES YANAHARIBU MASIKIO YAKO | Maisha Ni Afya
Breaking News
Loading...

Wednesday, February 5, 2014

MATUMIZI YA EARPHONES YANAHARIBU MASIKIO YAKO

[2 MB] BONYEZA HAPO CHINI KUPATA MICHONGO MIPYA YA AJIRA DAILY>>>>>>>>> !
Muziki unaosikiliza kwenye earphones unaweza kuwa na madhara kwenye masikio yako siku za usoni.Muziki wa kwenye earphones unaweza kusababisha ukashindwa kusikia vizuri au ukashindwa kusikia kabisa.Masikio yako yakishaharibiwa na earphones yanaweza yasirudie hali yake ya kawaida.
Earphones zinatusaidia bila shaka,lakini sauti ya juu sana unapoisikiliza kwa muda mrefu inasababisha kupotea kwa uwezo wa kusikia.Sauti ya juu huaribu kabisa chembe hai za masikioni zinazokufanya usikie.Chembe hai hizo zikiharibika hutaweza kusikia tena.
Pia muziki mkubwa wa kwenye disco au sherehe sio mzuri,lakini hatupati madhara kwa kuwa tunausikiliza mara chache tena kwa muda mfupi,.Wafanyakazi wa disco,club za usiku,studio za kurekodia muziki na viwanda vinavyopiga kelele ndio wapo hatarini kuathirika na aina hii ya kelele.
Kwenye nchi nyingi zilizoendelea kuna ongezeko kubwa la vijana wanaoripoti hospitali na tatizo la kutosikia,wengi kati ya vijana hao wamekiri matumizi ya muda mrefu ya earphones.Kama earphones zako zitakufanya uwe kiziwi,hakuna tiba itakayokusaidia.Epuka matumizi mabaya ya earphones.Sikiliza muziki kwa sauti ya chini,sikiliza kwa muda mfupi tu pale inapobidi.Kama unaweza acha kabisa matumizi ya earphones.
ANGALIZO
Kuna utata umejitokeza kuhusu uhusiano kati ya  matumizi ya earphones na madhara yake.Baaadhi ya tafiti zimethibitisha matatizo ya kusikia yatokanayo na aerphones,tafiti nyingine zimeshinwa kuthibitisha uhusiano kati ya matumizi ya earphones na matatizo ya kutosikia.Bila shaka tafiti zaidi zinahitajika.


[2 MB] BONYEZA HAPO CHINI KUONA NAFASI MPYA ZA KAZI KILA ZINAPOTOKA>>>>>>>>> !

google+

linkedin

MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI