Kutumia dawa na pombe wakati mmoja kunaweza kusababisha dawa uliyokunywa au kumeza ipungukiwe ufanisi wake au ishindwe kabisa kufanya kazi.Vile vile dawa na pombe vinaweza kutengeneza sumu hatari mwilini.
Mfano mzuri ni FLAGYL(flajili) dawa inayotumiwa kiholela na wengi kutibu kuharisha,flagyl kama itamezwa pamoja na pombe ndani ya dakika tano yafutayo humpata mtumiaji,presha ya damu hushuka,jasho jingi hutoka,kushindwa kupumua ,kifua kuuma na maumivu ya kichwa,kichefuchefu na kutapika.Ndani ya masaa machache mabaya zaidi hutokea,kifafa na mzunguko wa damu kusimama,hatimaye kifo hutokea kama hakutakuwa na juhudi zozote za kuokoa maisha.
Ulevi kwa upande mwingine unaweza kukufanya usahau kufuata dozi yako hivyo kuharibu tiba.Dawa zenye muingiliano na pombe ni nyingi mno kuzitaja moja moja,kama unaweza,epuka kutumia pombe ukiwa kwenye dozi au wasiliana daktari aliyekuandikia dawa kuhusu muingiliano wa dawa hiyo na pombe.
0 comments:
POST A COMMENT