Mwanamke huwa na uwezo wa juu wa kushika mimba anapokuwa mwanzoni mpaka katikati mwa miaka ya ishirini(mfano miaka 20 mpaka 25).Baada ya hapo uwezo wa kushika mimba huanza kupungua taratibu mpaka anapofikisha miaka 35.Lakini kuanzia miaka ya katikati ya thelathini(mfano 35) kuendelea mbele uwezo wa kushika mimba hushuka zaidi.Mojawapo ya sababu inayosababisha kupungua kwa uwezo wa kushika mimba kwa mwanamke kadri umri unavyoongezeka ni kupungua kwa ubora wa mayai yake.Lakini pia umri mdogo(mfano chini ya miaka ishirini) huwa sio mzuri kushika mimba kwa kuwa mwili wa binti unakuwa haujakomaa vya kutosha kuweza kuhimiri ujauzito,mfano nyonga inaweza kuwa haijatanuka vya kutosha kuweza kuruhusu mtoto kupita ukeni wakati wa kuzaa.
Tafiti hizi hazitakiwi kukuogopesha au kukufurahisha kwa sababu zifuatazo:
- Hazimaanishi kwamba ukiwa na umri mkubwa (mfano zaidi ya 35) basi hutoshika mimba,uwezo wa kushika mimba upo ila umepungua kidogo tu, wapo wanawake wengi walioshika na wanaoendelea kushika mimba wakiwa na umri mkubwa.
- Tofauti ya uwezo wa kushika mimba kati ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 34 na wale wenye umri kati ya 35 mpaka 40 iliyogunduliwa na watafiti siyo kubwa kiasi cha kuleta mashaka.
- Mbali na umri kuna sababu nyingine zinazobainisha uwezo wako wa kuzaa,mfano kuziba kwa mirija inayopitisha yai(fallopian tube) na uwezo wa mwanaume wako kukupa mimba.
- Kila mtu ni wapekee kwa aina yake,kuhukumu uwezo wako wa kuzaa kwa kuangalia tafiti walizofanyiwa watu wengine laweza kuwa jambo zuri lakini sio lazima liwe sahihi.
Wanawake ambao inasemekana kuwa umri umewaacha ndio haswa wapo kwenye nafasi nzuri kimalezi,akili zao zimetulia,wengi tayari wana njia za kuingiza pesa na mambo ya usichana yamepungua.Hawa wakishika mimba wanaweza kuwa walezi wazuri zaidi.
Fanya maamuzi yako ya kubeba mimba kwa usahihi,epuka presha ya aina yeyote,jipange vizuri.
0 comments:
POST A COMMENT