KUKOSA USINGIZI WA KUTOSHA
Kadri unavyotumia muda mfupi kulala wakati wa usiku ndio unavyojiongezea nafasi ya kuchoka na kuhisi usingizi mapema siku inayofuata.Usingizi unapumzisha mwili na akili yako.Lala kati ya masaa 6-8 kila siku.
MAZOEZI
Mazoezi ya asubuhi husisimua moyo,hufanya msukumo wa damu uwe na ufanisi zaidi,matokeo yake mwili mzima huchangamka.Fanya mazoezi utakayoyafanya kwa urahisi kama vile kuruka kamba,kuendesha baiskeli,kukimbia n.k
KUKOSA KIFUNGUA KINYWA SAHIHI
Kukosa kifungua kinywa(chai ya asubuhi) kutasababisha mwili wako ukose nguvu.Ubongo,moyo,misuli na viungo vingine mwilini mwako vinategemea chakula unachokula ili viweze kufanya kazi kwa ufasaha.Hakikisha unapata kifungua kinywa ili mwli wako uchangamke.Kupata kifungua kinywa ambacho sio sahihi kunaweza kusikusaidie.Hakikisha unapata mlo uliokamilika kila asubuhi.(Mada inayofuta kwenye blogu hii itahusu upangiliaji mzuri wa chakula,unakaribishwa kupitia)
UPUNGUFU WA MAJI MWILINI
Mwili wako unahitaji maji ya kutosha ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi.Ukosefu wa maji huzorotesha shughuli mbalimbali mwilini.Kunywa maji ya kutosha kila siku.Kipimo kizuri cha unywaji wako wa maji ni rangi ya mkojo wako,hakikisha mkojo wako unafana na maji au una rangi ya njano iliyopauka.
MAGONJWA
Kiujumla magonjwa kama malaria,maambukizi kwenye njia ya mkojo, kisukari n.k husababisha uchovu.Unaweza ukawa unahisi uchovu kwa sababu ya ugonjwa uliojificha.Unaweza kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo ili kujua afya yako.
ULAJI MBOVU
Baada ya kifungua kinywa asubuhi,mlo wako wa mchana na usiku una umuhimu katika kukuweka sawa.Usile chakula kingi sana kuliko shughuli unazofanya,pia usiwe mvivu kula.Chakula chako ni lazima kiwe cha mchanganyiko wa aina mbalimbali za vyakula vikiwemo wanga(ugali,wali n.k),protini(nyama,maharage n.k) mafuta(kiwango kidogosana),matunda na mboga za majani.
0 comments:
POST A COMMENT